Mama Kanumba afunguka hili juu ya Lulu - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 1 November 2018

Mama Kanumba afunguka hili juu ya Lulu

Mama Kanumba afunguka hili juu ya Lulu
Mama mzazi wa muigizaji Steven Kanumba, Bi. Flora Mtegoa, amefunguka juu ya chuki ambayo ilionekana wakati wa kesi iliyokuwa ikimkabili muigizaji, Elizabeth Michael, (Lulu) juu ya tuhuma za kumuua mwanae Steven kanumba.


Akizungumza na www.eatv.tv, Mama kanumba amesema kwamba hana chuki yoyote na Lulu, isipokuwa kama mzazi ambaye kapoteza mtoto, ndiyo maana alikuwa vile alivyoonekana.

“Kanumba mtoto wangu nilikuwa nampenda sana, ukizingatia mimi mwanangu nimemlea kwa tabu, mtu kamuua, mimi simchukii mtu, Lulu nampenda sana namtakia kila la heri, sijawahi kumchukia”, amesema mama Kanumba.

Ikumbukwe kwamba baada ya kifo cha Kanumba mama Kanumba alionekana bega kwa bega na Lulu ambaye ndiye alikuwa mtuhumiwa namba moja wa kifo chake, lakini baada ya kipindi kifupi kupita, kuliibuka mtafaruku mkubwa ambao chanzo chake hakikuwekwa wazi, mtafaruku uliosababisha wawili hao kufarakana na kuwa kama paka na panya.

No comments:

Post a Comment