ZITTO KABWE AKAMATWA KUHUSU TUHUMA ZA MAUAJI YA WANANCHI 100 - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 31 October 2018

ZITTO KABWE AKAMATWA KUHUSU TUHUMA ZA MAUAJI YA WANANCHI 100

MBUNGE wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kwa ajili ya mahojiano juu ya mauaji ya Polisi na raia yaliripotiwa kwenye Kijiji cha Mpeta, wilayani Uvinza mkoani Kigoma.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi, Mawasiliano ya Umma na Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu imesema kuwa kiongozi huyo amekamatwa na Polisi wa Kituo cha Osterbay jijini Dar es Salaam.

“Kiongozi wa Chama, ndugu Zitto Kabwe amekamatwa na Polisi wa Kituo cha Polisi Oysterbay muda huu kwa maelezo kuwa anakwenda kuhojiwa juu ya mauaji ya Polisi na raia yaliyotokea kwenye Kijiji cha Mpeta, wilayani Uvinza, mkoani Kigoma, mauaji ambayo Zitto alitaka Jeshi la Polisi liyatolee maelezo katika mkutano wake na Wanahabari juzi Jumapili, Oktoba 29, 2018”, amesema Shaibu.

Zitto amekamatwa ikiwa ni siku moja tangu Kamanda wa polisi mkoani Kigoma, Martin Ottieno katika mkutano wake na waandishi wa habari jana, alisema kuwa tuhuma alizotoa Zitto za mauaji ya wananchi 100 kwenye mapigano ya polisi na raia huko Uvinza, hazina ukweli wowote na kusisitiza kuwa ni upotoshaji unaofanywa na wanasiasa.

Hakuna watu mia moja waliouawa. Tunamtaka Zitto aonyeshe vielelezo vya hayo anayosema au aje atuonyeshe makaburi ya watu hao anaosema wameuawa Kigoma”, alisema Kamanda Ottieno.

No comments:

Post a Comment