Wapenzi wakutwa na viungo vya miili ya binadamu - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 9 October 2018

Wapenzi wakutwa na viungo vya miili ya binadamu

Polisi wanawashikilia wapenzi waliokuwa wanafanya biashara ya kusafirisha viungo vya binadamu ambavyo vina kadiliwa kuhusisha vifo vya watu 10.
Baada ya kuhojiwa na polisi mwanaume amekiri kuwa hadi sasa ameshawauwa watu takribani 20 ambao ni wanawake waishio mjini Mexico.
Wapelelezi wa kesi hiyo wamethibitisha kuwakuta wapenzi hao na ndoo zilizojaa viungo vya binadamu vilivyofunikwa kwa simenti na kugandishwa kwa barafu.
Na wamethibitisha kuwa walikuwa wanauza viungo hivyo kwa watu japo hawajatambua ni watu gani hununua viungo hivyo vya binadamu.
Mauaji ya wanawake nchini Mexico yanaongezeka kila siku na hakuna wanaokamatwa na kuwajibishwa, baada ya tukio hili maandamano yameanza mitaa ya watu wenye kipato cha chini, Ecatepec ambao mauaji yamekuwa yakitokea mara kwa mara.
Moja ya watuhumiwa Juan Carlos amekili kuuwa wanawake watatu na amesema kabla ya kuwaua alikuwa ana wabaka kwanza na kukata viungo vyao.
Mji wa Mexico umekuwa na matukio mengi ya kupotea kwa wanawake, kuanzia mwezi Januari watu 395 wameripotiwa kupotea na kati yao 207 ni wanawake.

No comments:

Post a Comment