Sakata la Picha za Uchi: RC Makonda Amtaka Amber Rutty Ajisalimishe Polisi Kabla ya Saa 12 Jioni - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 26 October 2018

Sakata la Picha za Uchi: RC Makonda Amtaka Amber Rutty Ajisalimishe Polisi Kabla ya Saa 12 Jioni

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam amemtaka msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Amber Rutty ajisalimishe polisi mwenyewe baada ya picha zake za utupu kuvuja mtandaoni.
RC Makonda

RC Makonda amemtaka msanii huyo aripoti kwenye kituo chochote cha Polisi kilicho karibu naye kabla ya saa 12 jioni.

“Wakati TCRA wakijipanga kuchukua hatua, mimi namtaka mwenye picha hii kufika kituo chochote Cha Polisi kilichopo karibu na eneo lake kabla ya 12 jioni. Na ukifika waambie umeitwa na RC Makonda watakupatia ujumbe wako.“amesema RC Makonda.

Siku ya jana kwenye mtandao wa Instagram kulisambaa video ya msanii huyo akiwa uchi wa mnyama akifanya mapenzi na jamaa yake, tena kinyume na maumbile.

Tukio hilo la kuvuja video hizo za utupu za Amber Rutty, limekuja masaa machache baada ya Muigizaji Wema Sepetu naye video zake za utupu kuvuja mtandaoni.

No comments:

Post a Comment