Mama Diamond Adai Kusubiri Kwa Hamu Harusi Ya Mwanaye - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 31 October 2018

Mama Diamond Adai Kusubiri Kwa Hamu Harusi Ya Mwanaye

Mama mzazi wa msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz. Bi. Sandra Kassimu au maarufu kama Mama Diamond ameibuka na kudai kuwa anasubiri kwa hamu harusi ya mwanaye huyo licha ya kwamba hana taarifa itafungwa lini.

Mama Diamond amefunguka na kuweka wazi kuwa licha ya kwamba anasubiri kwa hamu harusi hiyo lakini hajui tarehe ya mwananye kuoa na wala hajui ataoa mwanamke gani.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Risasi Vibes, mama Diamond alisema licha ya kwamba Diamond ni mwanaye, lakini hawezi kumchagulia mwanamke wa kuoa kwani hata yeye hakuchaguliwa mwanaume wa kuwa naye hivyo kikubwa anachosubiri ni kusherehekea tu siku hiyo.

Unajua siwezi kumchagulia Diamond  mwanamke wa kuoa bali yeye mwenyewe ndiye atakayechagua maana hata kama watu wanavyosema amuoe Zari (mzazi mwenza wa Diamond) wakati wanakutana na kuanzisha uhusiano wao mpaka wakapata watoto mimi sikuwepo hivyo mambo ya kuoa ni uamuzi wa mtu mwenyewe”.

Diamond ameshazaa watoto watatu na wanawake wawili tofauti lakini mpaka hivi sasa hajamuweka wazi mpenzi wake na kudai yupo single licha ya kuonekana na wanawake kadhaa na hata wanawake hao kumgombania hadharani.

No comments:

Post a Comment