Chelsea yalazimisha sare Stamford Bridge mbele ya vijana wa Mourinho - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 20 October 2018

Chelsea yalazimisha sare Stamford Bridge mbele ya vijana wa Mourinho

Vinara wa ligi kuu England klabu ya Chelsea imelazimishwa sare ya mabao 2 – 2 dhidi ya Manchester United kwenye uwanja wake wa nyumbani Stamford Bridge.
Katika mchezo huo wenyeji Chelsea ndiyo waliyokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 21 kupitia kwa mchezaji,  Anthony Ruediger kisha United kusawazisha bao hilo kupitia kwa Anthony Martial dakika ya 55 kipindi cha pili na kuongeza lingine 73 mpaka dakika 90 zinatimia vijana hao wa Mourinho walikuwa wakiongoza na katika dakika ya za nyongeza (90+6) Chelsea ikisawazisha bao hilo kupitia kwa Barkley na kufanya matokeo kuwa 2 – 2.
Kwa matokeo hayo Chelsea inaendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi kwakuwa na jumla ya pointi 21 wakati United ikiwa na alama 14 kwakuwa nafasi ya nane.

No comments:

Post a Comment