ZAHERA AZITAKA POINTI ZA SIMBA DAR, AFUNGUKA NAMNA HII - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 2 September 2018

ZAHERA AZITAKA POINTI ZA SIMBA DAR, AFUNGUKA NAMNA HII


Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga ameonesha dhamira ya kuutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu kwa kutaka kushinda mechi 10 mfululizo, imeelezwa.

Zahera amefunguka na kusema kwa sasa nguvu zote anazielekeza katika kuwaandaa vijana wake ili kuhakikisha wanaanza vema zaidi baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kocha huyo ameeleza malengo yao ni kuhakikisha wanapata alama 30 ikiwemo zile za Simba watakapokutana Septemba 30 2018 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mkongomani huyo ana imani kubwa ya kikosi chake kuimarika kutokana na upinzani walioupata kutoka kwenye mashindano ya kimataifa baada ya kucheza na vigogo kama USM Alger na Gor Mahia FC ya Kenya.

Kwa sasa kikosi cha Yanga kimezidi kujifua kwa ajili ya mechi za ligi kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment