YANGA YAANIKA HADHARANI WACHEZAJI WOTE WALIO MAJERUHI MPAKA SASA - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 10 September 2018

YANGA YAANIKA HADHARANI WACHEZAJI WOTE WALIO MAJERUHI MPAKA SASA


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Yanga umefunguka kuhusiana na wachezaji wake mabo bado hali zao hazipo sawa kiafya.

Kwa mujibu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, imewataja Abdallah Shaibu, Juma Abdul na Juma Mahadhi ndiyo ambao bado hali zao hazijakaa sawa kutokana na kuwa majeruhi ambapo mpaka sasa wanaendelea na matibabu.

Wachezaji hao wote walikosekana kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya African Lyon ambapo Yanga ilibuka na ushindi wa bao 1-0.

Aidha, beki Kelvin Yondani naye bado hajawa fiti baada ya kuumia akiwa na kikosi cha Stars na kupelekea kuikosa safari ya kuelekea Uganda kwa ajili ya mechi ya kufuzu kuelekea AFCON.

Yanga wamesema uwezekano wa wachezaji wake majeruhi kurejea kikosini upo kwa siku za hivi karibuni kutokana na maendeleo yao kwenda vizuri.

No comments:

Post a Comment