YANGA WATAKA MCHEZAJI WAO AFUTWE KAZI - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 17 September 2018

YANGA WATAKA MCHEZAJI WAO AFUTWE KAZI


Licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Stabd United, mashabiki wengi wa klabu ya Yanga wameutaka uongozi kumfuka kazi kipa wake Mkongo, Klaus Kindoki.

Mashabiki hao wenye hasira (majina tunayo) wameeleza kutofurahishwa na uwezo wake baada ya kuruhusu mabao matatu.

Kitendo cha Kindoki kufungwa mabao hayo ambayo wameeleza kuwa yalikuwa laini, kimewaumiza baada ya kupoteza mvuto wa ushindi wao ingawa wamepata alama tatu.

Kindoki aliweza kuruhusu mabao hayo na kumpa zawadi straika Alex Kitenge ambaye aliondoka na mpira kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Uwezo wa Kindoki umewaweka njia panda mashabiki hao ambao wengi wao wameona hana uwezo wa kuicheza Yanga la sivyo awekwe benchi kwa muda mpaka pale atakapojifunza.

Baada ya ushindi dhidi ya Stand, Yanga sasa wataanza maandalizi ya kujiandaa na mechi dhidi ya Coastal Union ya Tanga ambayo watacheza nayo Uwanja wa Taifa Jumatano ya wiki hii.

No comments:

Post a Comment