WANACHAMA SIMBA WAIKATAA KATIBA MPYA, WAELEZA SABABUa - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 11 September 2018

WANACHAMA SIMBA WAIKATAA KATIBA MPYA, WAELEZA SABABUa


Wakati zoezi la kurudisha fomu za wagombea nyadhifa mbalimbali katika klabu ya Simba likianza leo Jumanne, baadhi ya wanachama wameitaka katiba ya 2014 kutumika.

Wanachama hao wameeleza kuitaka katiba hiyo wakiamini ndiyo imefauata haki zote za wanasimba tofauti na mpya iliyopitishwa 2018.

Mwanachama mmoja ambaye hajataka jina lake liwekwe hadharani, amesema katiba ya 2018 ilipitishwa kiujanja ujanja kwa lengo la kuwanufaisha baadhi ya watu.

Aidha, Mwanachama huyo amefunguka kwa kusema katiba hiyo ina vipengele ambavyo vinawabana baadhi ya wanaotaka kugombea nafasi ndani ya uongozi ikiwemo suala ya kuwa na digrii badala ya elimu ya kidato cha nne.

Ukiachana na Mwanachama huyo aliyepinga, wanachama wengine wameonesha kuiunga mkono katiba mpya ambayo ndiyo itatumika kwa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Novemba 3 2018.

Wanachama hao wameeleza katiba hiyo itawafungulia milango mizuri kuelekea mfumo wa muundo mpya ambao Simba inaelekea kuuanza rasmi ikiwa chini ya Mwekezaji.

No comments:

Post a Comment