VAN DER SAR, OZIL, SHAW, GAYLE, DE JONG: TETESI KUBWA ZA SOKA ULAYA LEO JUMANNE - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 11 September 2018

VAN DER SAR, OZIL, SHAW, GAYLE, DE JONG: TETESI KUBWA ZA SOKA ULAYA LEO JUMANNE


Kiungo wa kati wa Arsenal Mjerumani Mesut Ozil, 29, anawindwa na klabu ya Uturuki ya Fenerbahce. (Fotomac)

Tottenham wanamfuatilia beki wa Leicester City mwenye miaka 21 Ben Chilwell, ambaye ameitwa kwenye kisosi cha England na ambaye amepangwa kwa ofa ya mchezaji wa Ajax raia wa uholanzi Frenkie de Jong, 21. (Telegraph)

Mshindi mara nne wa Ligi ya Premio Edwin van der Sar, 47, amesema hajiungi katika kikosi cha kiufundi huko Manchester United.(Sky Sports)


Chelsea ililipa zaidi kwa karibu pauni milioni 40 wakati ilitumia pauni milioni 7 kwa kipa wa Athletic Bilbao mwenye miaka 23 Kepa Arrizabalaga mwezi Agosti kwa mujibu wa shirika la uanngalizi wa kandanda CIES. (Football Italia)

Kiungo wa kati wa Charlton Athletic mwenye miaka 16 Jeremy Sarmiento, ambaye alizaliwa huko Madrid kwa wazazi kutoka Ecuador anakaribia kujiunga na klabu ya Ureno ya Benfica licha ya Manchester City kumwinda. (London Evening Standard)


Mlinzi wa Manchester United Luke Shaw, 23, huenda akakosa mechi mbili ya klabu chake baada ya kupata jheraha akiichezea England. United watacheza na Watford siku ya Jumapili kabla ya kusafiri kwenda Uswizi kukutana na Young Boys kwenye ligi ya mabingwa Jumatano ijayo. (Mirror)

West Bromwich Albion hawawezi kumpoteza mshambuliaji Dwight Gayle, 28, msimu huu licha ya ripoti kuwa vilabu vya China vinanammezea mate mshambuliaji huyo. Gayle yuko kwenye mkopo wa msimu wote kutoka Newcastle United. (Express & Star)


Fainali ya ligi ya mabingwa itaandaliwa mjini New York siku za usoni, kwa mujibu wa mfanyabiashara mmoja. Kuanzia mwaka 2021 na kuendelea, hakuna maeneo yaliyoathiriwa kwa fainali hizo. (Sun)

Kutoka BBC

No comments:

Post a Comment