TETESI KUBWA ZA SOKA BARANI ULAYA LEO JUMAPILI YA SEPTEMBA 30 2018 - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 30 September 2018

TETESI KUBWA ZA SOKA BARANI ULAYA LEO JUMAPILI YA SEPTEMBA 30 2018


Machester United wanaamini kuwa meneja Jose Mourinho anaweza kufutwa kazi mwishoni wa wiki ijayo huku wachezaji wakizungumzia uwezekano wake kufutwa walipokuwa wakirudi nyumbani baada ya kushindwa kwa mabao 3-1 na West Ham siku ya Jumamosi. (Mail on Sunday)

Mourinho amwambia Pogba kuwa hakuna mchezaji mkubwa kuliko timu
Lakini United wanasema ripoti kuwa wamezungumza na meneja wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane kuchukua mahala pake Mourinho ni upuzi. (ESPN)

Mourinho alimkosoa mshambuliaji wa United Mchile Alexis Sanchez, 29, mbele ya wachezaji wenzake kabla ya kumtoa kutoka kwa kikosi kilichocheza Jumamosi. (Sunday Mirror)


Barcelona wanamtaka kiungo wa kati wa United Paul Pogba, ambaye aliambia wiki hii kuwa hawwezi kuwa nahodha wa Manchester United tena lakini wanaweza kumsaini mchezaji huyo wa miaka 25 msimu ujao badala ya mwezi Januari. (Sunday Express)

Manchester City wanataka kuvunja rekodi ya kununua wachezaji kwa kumsaini mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, 19 kwa pauni milioni 200. (Sun on Sunday)

Mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata, 25, atauzwa kweda Juventus mwezi Januari. (Sun on Sunday)

Chelsea wanamfuatilia ndugu wa miaka 15 wa mshambuliaji Mbeljii Eden Hazard, 27, na kiungo wa kati Kylian, 23. Ethan Hazard anaichezea klabu ya Ubelgiji ya AFC Tubize. (Sunday Mirror)


Cristiano Ronaldo anaamini bao lake dhidi ya Juventus akiwa na Real Madrid lilikuwa bora zaidi kuliko la Mohammed Salah lililomshindia mshambuliji huyo wa Liverpool tuzo ya Fifa la Puskas Award. Lakini mreno huyo aliongeza kuwa Salah, 26 alistahli tuzo hiyo. (L'Equipe - in French)

Kipa wa Liverpool Alisson, 25, anasema mchezaji mwenzake Philippe Coutinho - ambaye aliondika Anfield na kujiunga na Barcelona mwezi Januari - alimsaidia kuamua kujiunga na Ligi ya Premier. (Goal)

Kutoka BBC

No comments:

Post a Comment