TETESI KUBWA ZA SOKA BARANI ULAYA LEO JUMAPILI - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 23 September 2018

TETESI KUBWA ZA SOKA BARANI ULAYA LEO JUMAPILI


Kiungo wa kati Jack Grealish, 22, anatarajiwa kukataa ofa ya Tottenham na kusaini mkataba zaidi na Aston Villa. (Express)

Mwenyekiti wa Juventus Andrea Agnelli anataka mabingwa hao wa Italia kumsaini wing'a wa Manchester City mjerumani Leroy Sane, 22. (Calciomercato)

Mshambuliaji wa zamani wa LA Galaxy raia wa Sweden Zlatan Ibrahimovic, 36, amepewa ofa ya kurudi klabu yake ya utotoni ya Malmo. (Sun)

Manchester City wanatajiunga na Manchester United katika mbio za kumasaini kiungo wa kati mholanzi Frenkie de Jong, 21. (Mirror)

City pia wataka kumsani tena kiungo wa kati wa Paris St-Germain Adrien Rabiot, 23, ambaye alikuwa na muda mfupi huko Etihad kama kijana na ambaye anatarajiwa klabua hiyi ya Ufaransa msimu ujao. (Star)


Mshambuliaji wa Ajax raia wa Brazil David Neres, 21, amehusishwa na Tottenham na Roma. (De Telegraaf, via Calciomercato)

Fulham wanatarajiwa kutoa ofa ya pauni milioni 18 kwa mshambuliaji wa Lyon raia wa Ivory Coast Maxwel Cornet, 21. (Sun on Sunday)

Arsenal walikataa fursa ya kumsaini mlinzi wa Liverpool Virgil van Dijk, 27, akiwa huko Cletic kwa sababu mholanzi huyo alikuwa mtulivu sana. (Bein Sports, via Metro)


Mlinzi wa Manchester City Kyle Walker, 28, anasema anataka kurudi nafasi yake ya beki na England baada ya kucheza kama kiungo cha kati na nyuma wakati wa kombe la dunia. (Mail on Sunday)

Kutoka BBC

No comments:

Post a Comment