Tamasha la mbio za magari ya kizamani yanachangia pesa kwa watoto yatima Z'bar - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 2 September 2018

Tamasha la mbio za magari ya kizamani yanachangia pesa kwa watoto yatima Z'bar


Na.Thabit Madai, Zanzibar.

Waziri wa Habari na Mambo ya kale Mahmoud Thabit Kombo amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea na Juhudi za Kuthamini na kuunga mkono mchango na harakati zinazofanywa na Tasisi binafsi katika kukuza utalii wa Zanzibar.

Alisema kuna Taasisi nyingi za binafsi ndani na nje ya nchi zimekuwa zikitoa mchango mkubwa kutokana na harakati wanazozifanya za kutambulisha utamaduni mbali mbali uliopo Zanzibar na kupelekea kukuza sekta ya utalii wa ndani Zanzibar.

Hayo aliyabainisha wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Tamasha la mbio za magari ya kizamani yaliyotumiwa Zanzibar ambapo tamasha hilo limeandaliwa na hotel ya Park hayyat, hotel ya Melia na Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri Kombo alisema hatua iliyochukuliwa na hotel ya Park hayyat pamoja na Hotel ya melia kuanzisha na kuendeleza  Tamasha hilo la matembezi na mbio za magari ya kizamani ni kuunga mkono utekelezaji kwa  vitendo sera ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ya kukuza utalii wa ndani na kuongeza watalii hadi kufikia laki tano kwa mwaka.

Aidha alisema mbio hizo mbali ya kuwa lengo la kukuza utalii wa ndani na kuongeza idadi ya watalii bali kwa mwaka huu yamekuja na lengo la kukusanya fedha na kuwasaidia watoto mayatima wanaoishi katika nyumba ya kulelea watoto Mazizini.

Hata hivyo Waziri Mahoud Thabit Kombo serikali ya Zanzibar ipo katika hatua kuimarisha mifumo ya Takwimu Kwa uingiaji wa wageni nchini ili kujua takwimu sahihi za wageni wanaiongia Zanzibar.

Nae Waziri wa Kazi Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Moudile cylus kastiko alisema amefarijika kuona kwa  Tamasha hilo ambapo lipo kwa lengo la kukuza utalii wa ndani wa Zanzibar na kuchangia maendeleo ya Zanzibar.

“Nadhani tamasha hili limekuja wakati muafaka ambapo wananchi watapata kujifunza kwa kuona historia ya magari ambayo yametumiwa Zanzibar” alisema wazir kastiko.

Hata hivyo alisema tamasha hilo likiendelezwa litapunguza tatizo la ajira nchini kwa kufungua fursa za ajira mbali mbali kwa vijana kuweza kuajiriwa na kujiajiri katika sekta hiyo ya utalii.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa hotel ya Park Hayyat alisema Mbio hizo za magari kwa mwaka huu yameshirikisha wadau mbali mbali katika sekta ya utalii nchini wakimwemo watembeza utalii, hospitali za bianfsi, mashirika ya ndege pamoja na wadau wengine.

Aidha aliomba serikali kuchukua juhudi za kutafuta magari ya kuzamani yaliyotumiwa Zanzibar kwa lengo la kuyafufua na kutumika katika matamasha kama hayo kwa miaka inayokuja.

Mbio hizo za magari ya kizamani yameanza mji mkongwe katika Hotel ya park hayyat, kituo cha kulelea watoto yatima Mazizi na kumalizikia katika Hotel ya melia iliyopo kiwengwa mkoa wa kaskazini Unguja.

No comments:

Post a Comment