SUAREZ, POGBA, MORATA, PELLEGRIN: TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATANO - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 5 September 2018

SUAREZ, POGBA, MORATA, PELLEGRIN: TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATANO


Luiz Suarez anasema Paul Pogba atakaribishwa huko Barcelona wakati mchezaji huyo wa miaka 25 wa Manchester United anazidi kuhusishwa na kuhama kutoka Old Trafford. (ESPN)

Lakini pia Pogba anataka kucheza chini ya usimamizi wake Zinedine Zidane siku za usoni, wakati ripoti zikesema kuwa United wanaweza kumwinda meneja huyo wa zamani wa Real Madrid kuchukua mahala pake Jose Mourinho. (Metro)

Vilabu vikubwa saba vikiwemo wa ligi ya Premio, Manchester City, Chelsea, Manchester United na Liverpool-vimetumia zaidi ya dola bilioni moja kuwanunua wachezaji tangu mwaka 2010. (Daily Mail)

Meneja wa Real Madrid Julen Lopetegui amepuuzilia mbalia ya kuhama wachezaji wa Paris St-Germain Neymar, 26, na Kylian Mbappe, 19. (Express)

Mlinzi wa kikosi cha Ufaransa kilichoshinda Kombe la Dunia Benjamin Pavard, 22, anasema hajafikia makubaliano yoyote ya kujiunga na Bayern Minich kutoka Stuttgart. (Sky Sports)

Mchezaji wa miaka 25 Mhispania Alvaro Morata anasema msimu uliopita ulikuwa mgumu kwake. (Marca - in Spanish)

West Ham watamlipa Manuel Pellegrini pauni milioni 15 ikiwa watamfuta meneja huyo wao raia wa Chile. (Times - subscription required)

Nyota wa Spurs na England Dele Alli, 22, amefichua jinsi mkufu aliopewa na dereva wa teksi nchini Urusi ulichangia awe na bahati nzuri. (Standard)

Ligi ya Premio inataka serikali kufuta vuzuizi vyote vya kuwasaini wachezaji wa kigeni kufuatia hofu kuwa Brexit itaathiri umaarufu wa ligi hiyo. (Telegraph)

Kutoka BBC

No comments:

Post a Comment