Shilole Ampa Neno Diamond....."Ndo Maana Wanawake Wanakuroga" - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 6 September 2018

Shilole Ampa Neno Diamond....."Ndo Maana Wanawake Wanakuroga"

Bado kile kinachodaiwa kuwa Hamisa Mobetto alitaka kumloga Diamond Platnumz na familia yake kinazidi kuchukua nafasi kwenye mitandao ya kijami.

Mjadala umekuwa mpana hasa kwa kauli aliyoitoa jana Diamond kupitia Wasafi TV ingawa upande wa Hamisa amekuwa kimya kwenye suala hilo.

Sasa muimbaji Shilole hajawa nyuma kwenye hilo ameposti picha ya Diamond Platnumz (ipo chini) na kuisindikizia na caption iliyosema; 'Ndio maana wanakuroga, medamshi sana kaka yangu Diamond Platnumz,'.

Mwanamitindo Hamisa Mobetto amezaa mtoto mmoja na Diamond Platnumz na utakumbuka hadi muimbaji huyo anakiri kuwa amezaa na Hamisa ilikuwa ni baada ya mvutano mrefu na hii ni kutokana kipindi hicho Diamond bado alikuwa na mahusiano na Zari.

No comments:

Post a Comment