SHAMRA SHAMRA ZA MAADHIMISHO YA 16 YA SIKU YA TIBA ASILI YA KIAFRIKA - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 2 September 2018

SHAMRA SHAMRA ZA MAADHIMISHO YA 16 YA SIKU YA TIBA ASILI YA KIAFRIKA

Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Amina Salum Ali akitoa hutuba yake katika kilele cha Maadhimisho ya 16 ya siku ya Tiba asili Afrika.  Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya afya Zanzibar Dkt. Mayasa Salum Ali na kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Mzee Mohamed Kheri. Maadhimisho hayo yalifanyika Ukumbi wa Shekh Idrisa Abdul Wakili Kikwajuni mjini Zanzibar. Picha na Abdalla Omar-Maelezo Zanzibar.   
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya afya Zanzibar Dkt. Mayasa Salum Ali akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya 16 ya siku ya Tiba asili Afrika yalifanyika Ukumbi wa Shekh Idrisa Abdul Wakili Kikwajuni mjini Zanzibar. Picha na Abdalla Omar-Maelezo Zanzibar.   
Wanafunzi wa Madarasat Altawakal kutoka Magomeni mjini Zanzibar wakitumbuiza Dufu ikiwa ni shamrashamra za kilele cha Maadhimisho ya 16 ya siku ya Tiba asili Afrika.


 Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Amina Salum Ali akiangalia Dawa asili kutoka kwa Vikundi mbalimbali vya Wajasiriamali waliofika Zanzibar kushiriki Maadhimisho ya 16 ya siku ya Tiba asili Afrika ambapo kwa Zanzibar yalifanyika Ukumbi wa Shekh Idrisa Abdul Wakili Kikwajuni mjini Zanzibar. Picha na Abdalla Omar-Maelezo Zanzibar 
Na Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment