Serikali yatoa mafunzo kwa wanahabari jinsi ya kuepukana na Ebola - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 3 September 2018

Serikali yatoa mafunzo kwa wanahabari jinsi ya kuepukana na Ebola


WAANDISHI wa Habari wametakiwa kushirikiana na Serikali katika kuihabarisha jamii ili kuepukana na janga hatari la ugonjwa wa Ebola.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  ameyabainisha hayo wakati wa kufungua mafunzo maalum kwa waandishi wa namna ya kutoa taarifa za ugonjwa huo wa Ebola.

Jamii imetakiwa kujua dalili za ugonjwa huo wa Ebola kwa kina kwani kupitia Wanahabari,mafunzo hayo yatasaidia sana kutoa elimu na itaenea maeneo mengi.

“Ugonjwa huu wa Ebola kiukweli ni ugonjwa hatari. Na tokea kutokea katika nchi za wenzetu umesababisha madhara makubwa sana ikiwemo Uchumi ikiwemo masuala ya biashara na uwekezaji.

Imebainishwa kuwa madhara ya kiuchumi juu ya Ebola yangeuwa watu wengi zaidi kuliko ugonjwa wenyewe. Sisi tulikuwa na wasiwasi sana ndio maana tulienda wenyewe huko kufuatilia..mimi nilienda mipakani Rusumo na Mganga Mkuu yeye alienda mipaka ya Ngala na maeneo mengine.” Amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Na kuongeza kuwa, tatizo kubwa ni suala la wasafiri wanaopita njia za panya kwani zimekuwa zikiwapa changamoto na wameomba Kamati za Ulinzi na Usalama kuhakikisha wanalinda maeneo hayo.

No comments:

Post a Comment