Samatta, wenzake kujiunga Stars leo - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 3 September 2018

Samatta, wenzake kujiunga Stars leo

MBWANA SAMATTA.

WACHEZAJI wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)akiwamo Mbwana Samatta, wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi wanatarajiwa kuanza kuwasili leo kwa ajili ya kujiunga na kambi ya timu hiyo kujiandaa na mechi ya kuwania kufuzu Afcon dhidi ya Uganda itayokayopigwa Septemba 8, mwaka huu.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford  Ndimbo alisema jana kuwa wachezaji wanaotarajiwa kujiunga na timu hiyo mbali na Samatta anayeichezea KRC Genk ya Ubelgiji, ni Thomas Ulimwengu (El Hilal, Sudan), Simon Msuva( Difaa Hassan EL Jadida, Morocco), Farid Musa (CD Tenerife Hispania), Rashid Mandawa(BDF xi, Botswana), Himid Mau (Petro Jet FC, Misri), Shabani Idd Chilunda (CD Tenerife, Hispania), Hassan Kessy (Nkana FC, Zambia), Abdi Banda (Baroka FC, Afrika Kusini).

Kikosi cha Taifa Stars jana kiliendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa kikiwa chini ya Kocha Mkuu Mnaigeria Emmanuel Amunike.

No comments:

Post a Comment