RONALDO, MOURINHO, BECKER, MOURINHO: TETESI KUBWA ZA SOKA ULAYA LEO JUMATATU - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 3 September 2018

RONALDO, MOURINHO, BECKER, MOURINHO: TETESI KUBWA ZA SOKA ULAYA LEO JUMATATU


Kocha wa West Ham Manuel Pellegrini hayupo kwenye hatari ya kufurushwa na waajiri wake licha ya kupokea vichapo vine mfululizo. (Mirror)

Kipa raia wa Uhispania David de Gea, 27, anatarajia kusaini mkataba mpya na klabu yake ya Manchester United ambapo atapokea mshahara wa £350,000 kwa wiki. (Sun)

Mshambuliaji wa klabu ya Paris St-Germain na timu ya Taifa ya Brazil Neymar, 26, adaiwa kupendelea kujiunga na Chelsea ama Arsenal lakini si timu mbili hasimu za jiji la Manchester. (Express)

Kiungo wa klabu ya Tottenham na nchi ya Ubelgiji Mousa Dembele, 31, anatarajiwa kwenda kusakata kabumbu Uchina mwezi Januari kwenye dirisha dogo la usajili. (Sun)

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema suala la Cristiano Ronaldo kurudi Old Traford wala hailkuwepo kwenye meza ya mazungumzo. Rodaldo amejiunga na Juventus akitokea Real Madrid. (Sky Sports)

Cristiano Ronaldo bado hajaifungia goli Juventus lakini mtoto wakw mwenye miaka nane mwisho wa juma liliopita amepachika magoli manne kwenye moja ya timu za watoto za klabu hiyo. (Marca)

Mlinzi wa klabu ya Arsenal na Ujerumani Shkodran Mustafi anaweza akaadhibiwa na Chama cha Mpira (FA) kwa namna alivyoshangilia goli lake dhidi ya Cardiff siku ya Jumapili. (Mirror)


Uhusiano wa kocha wa Manchester City Pep na winga Leroy Sane, 22, kumewaogofya wachezaji wengine wa timu hiyo, hususan katika kupata nafasi ya kucheza. (London Evening Standard)

Kutoka BBC

No comments:

Post a Comment