MZEE AKILIMALI AMUIBUKIA FEI TOTO, TAMKO LAKE HILI HAPA - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 17 September 2018

MZEE AKILIMALI AMUIBUKIA FEI TOTO, TAMKO LAKE HILI HAPA


Katibu wa Baraza la Wazeee wa Yanga, Ibrahim Akilimali, amesme jana hakufurahishwa na ufundi wa kiungo wa timu yake, Feisal Salum 'Fei Toto' katika mchezo dhidi ya Stand United..
Akilimali ameeleza hayo baada ya mchezo huo kumalizika kwa matokeo ya ushindi wa mabao 4-3 na kuifikishia Yanga alama 6 ikishinda mechi zote mbili za ligi.

Katibu huyo anaamini bado kiungo kiungo huyo ataendelea kwa vizuri kwa mechi zijazo ingawa kwa jana hakufurahishwa na namna uchezaji wake ulivyokuwa.

Aidha, Akilimali ameshauri Toto kuendelea kupambana ili kujitengenezea njia za kulisongesha soka lake nje ya Tanzania ili kutimiza ndoto zake kwa uwezo alionao ndani ya Uwanja.

Toto alisajiliwa na Yanga akitokea JKU ya Zanzibar na kusaini mkataba wa miaka miwili huku usajili wake ukigubikwa na zengwe baada ya Singida United kudai walikuwa wameshamalizana naye.

No comments:

Post a Comment