Mwili wa Mtoto Mdogo Waopolewa Leo Wakati Shughuli ya Kunyanyua Kivuko Ikiendelea... - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 25 September 2018

Mwili wa Mtoto Mdogo Waopolewa Leo Wakati Shughuli ya Kunyanyua Kivuko Ikiendelea...Idadi hiyo imefikia baada ya Mwili wa mtoto mmoja kuopolewa leo ambapo shughuli ya kukivuta Kivuko hicho inaendelea

Itakumbukwa kuwa jana Septemba 24 miili ya watu wawili iliopolewa katika eneo la ajali hiyo kwenye Ziwa Victoria

Aidha, baada ya kufanikiwa kukilaza kwa ubavu Kivuko hicho baadhi ya mizigo ikiwamo mikungu ya ndizi, mikoba na majamvi imeanza kuelea na kusukumwa na maji hadi ufukwe wa kijiji cha Bwisya katika kisiwa cha Ukara

Kazi ya kunyanyua kivuko hicho kilichozama Septemba 20 na kujifunika inafanywa na wataalam kutoka JWTZ na vikosi vingine vya ulinzi na usalama wakishirikiana na Maafisa kutoka kampuni ya Songoro Marines ya jijini Mwanza

No comments:

Post a Comment