MTIBWA WAZITAKA FEDHA ZA KOMBE LA FA HARAKA, BADO HAWAJAPEWA - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 11 September 2018

MTIBWA WAZITAKA FEDHA ZA KOMBE LA FA HARAKA, BADO HAWAJAPEWA


Uongozi wa klabu ya Mtibwa Sugar umeibuka na kueleza kuwa mpaka sasa haujapokea fedha zake za ubingwa wa Kombe la Shirikisho 'Azam Sports Federaton Cup'.

Kwa mujibu wa Msemaji wa timu hiyo, Thobias Kifaru amesema klabu hiyo haijapokea fedha zake tangu kuchezwa kwa fainali hiyo Juni 2 2018 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Kifaru amefunguka kwa kueleza kuwa haelewi mpaka sasa sababu za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutofanya mpango wa kuwapatia fedha zao haraka kwa maana ni mezi takribani mitatu sasa imekatika.

"Hatujakabidhiwa fedha zetu mpaka sasa, hatulewi tatizo lipo wapi, nadhani TFF wanapaswa kuliangalia hili haraka watukabidhi" alisema.

Mtibwa walifanikiwa kutwaa ubingwa huo baada ya kuilaza Singida United kwa mabao 3-2 na kuweka historia ya kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza.

No comments:

Post a Comment