Msemaji wa Jeshi la Polisi Uganda mwenye ukaribu zaidi na Bobi Wine auawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 10 September 2018

Msemaji wa Jeshi la Polisi Uganda mwenye ukaribu zaidi na Bobi Wine auawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana

Aliyewahi kuwa Msemaji wa jeshi la polisi mjini Buyende, Muhammad Kirumira ambaye pia amekuwa karibu na msanii wa muziki nchini humo, Bobi Wine ameuawa na watu wasiojulikana akiwa nyumbani nyumbani kwake jana Jumamosi Septemba 8, 2018.

Kamanda Muhammad Kirumira (kushoto) akiwa na Bobi Wine
Kufuatia kifo hicho, Bobi Wine ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kyadondo ametuma salamu za rambi rambi kwa familia yake na kueleza ukaribu wake na Muhammad kupitia ukuarasa wake wa Twitter.
Am so saddened by the terrible news of the shooting of my good friend, and outspoken police officer, Muhammad Kirumira. Very sadly, that is the country we are living in. NO ONE IS SAFE. Our country is bleeding. This is very painful.


Tayari Jeshi la Polisi nchini Uganda limethibitisha taarifa hizo na limeahidi kuanza kufanya upelelezi kwa kina kuwapata wahalifu wa tukio hilo.Imeelezwa kuwa watu hao waliotekeleza shambulizi hilo walikuwa kwenye boda boda. Mwaka jana mwezi Marchi aliyekuwa msaidizi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Uganda, Andrew Felix Kaweesi alishambuliwa na kuuawa katika eneo hilo hilo na watu wasiojulikana.

No comments:

Post a Comment