MESSI ASHANGAZWA NA MAAMUZI HAYA YA RONALDO - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 4 September 2018

MESSI ASHANGAZWA NA MAAMUZI HAYA YA RONALDO


Mshambulizi wa Barcelona mwenye miaka 31 raia wa Argentina Lionel Messi amesema alishangazwa na uamuzi wa mshambuliaji mwenye miaka 33 wa Real Madrid Cristiano Ronaldo kuondoka Real Madrid kwenda Juventus.

Kwa mujibu wa jarida la AS, Messi ameeleza kushangazwa na uamuzi wa nyota huyo ambaye alikuwa tegemeo kubwa ndani ya kikosi cha Madrid .

Messi anaamini endapo Ronaldo angeendelea kusalia Madrid angeweza kuleta ushindani mkubwa zaidi kwenye La Liga na baina ya timu hizo mbili hasa kwenye mechi ya El Clasico iliyo na ukubwa wa aina yake.

Ronaldo kwa sasa tayari ameshajiunga na Juventus ya Italia na tayari ameshacheza mechi takribani tatu za ligi hiyo ya Seria A.

No comments:

Post a Comment