Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu watua nchini kimyakimya kuikabili Uganda ‘The Cranes’ - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 4 September 2018

Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu watua nchini kimyakimya kuikabili Uganda ‘The Cranes’

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Mbwana Samatta anayecheza katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji na mshambuliaji wa Al Hilal ya Sudan, Thomas Ulimwengu wametua nchini alfajiri ya leo.
Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wametua nchini ili kujiunga na kambi ya timu ya Taifa inayojiandaa na mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu Afcon dhidi ya Uganda.
Baadhi ya nyota wengine wanaocheza nje ya nchi na kuwasili ni Rashid Mandawa na Ramadhani Kessy.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa Mandela uliyopo Namboole Uganda utakao fanyika Septemba 8 ya mwaka huu 2018.

No comments:

Post a Comment