Man Fongo akamatwa na Polisi - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 20 September 2018

Man Fongo akamatwa na Polisi

Man Fongo

Baba mzazi wa msanii wa miondoko ya singeli, Man Fongo amedai haelewi sababu iliyosababisha kukamatwa kwa mtoto wake huyo 'week end' hii, licha ya kuwa inadaiwa amekamatwa kutokana na kuvuta bangi.

Akizungumza na eNewz, baba mzazi wa Man Fongo amesema yeye alipewa taarifa kuwa mwanaye amekamatwa na madai yakiwa ni kukutwa na bangi japo anajuwa kuwa mwanaye anatumia sigara tu.

"Kuna kitu kinatengenezwa dhidi ya Man Fongo sio bure maana mtu akishakuwa maarufu basi watu hupenda kuwa haribia na kuwachafua kwa baadhi ya vitu. Nilienda kituo cha Polisi cha Ali Maua na nilipofika hapo, nikaulizwa na askari kuwa wewe ndio mzazi wa Man Fongo, nikamjibu ndio kisha yule askari akaniambia mwanao mimi nitamharibia", amesema baba wa Man Fongo.

Mbali na hilo, baba huyo amesema wakati alipokuwa anakamatwa Man Fongo pia alichukuliwa mdogo wake kwa kile kilichodaiwa kuwazuia askari wasimkamate ndugu yake.

No comments:

Post a Comment