Majibu ya Mimi Mars kwa Whozu Anayevizia Penzi Lake - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 4 September 2018

Majibu ya Mimi Mars kwa Whozu Anayevizia Penzi Lake

Msanii wa muziki Bongo, Mimi Mars amejibu kile alichoanzisha Whozu.

Utakumbuku kuwa msanii Whozu alieleza kuwa amekuwa akivutiwa zaidi kimapenzi na Mimi Mars na alishawahi kumueleza hilo.

"Dah!! Whozu kaamua kujitoa fahamu, nimemwambia nitamfikiria," Mimi Mars amejibu hivyo alipoulizwa na Wasafi TV.

Whozu si msanii wa kwanza kueleza hisia zake wazi wazi kwa Mimi Mars, hata Frend wa Makomando alishafanya hivyo ingawa mrembo huyo anaeleza kutokuwa tayari kwa hilo. Mimi Mars kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao Kodoo.

No comments:

Post a Comment