Luka Modric avunja ufalme wa Messi na Ronaldo - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 25 September 2018

Luka Modric avunja ufalme wa Messi na Ronaldo

Luka Modric akizungumza baada ya kushinda tuzo

Nyota wa Real Madrid na Croatia, Luka Modric ametangazwa mchezaji bora wa dunia wa FIFA mwaka 2018 kwenye tuzo zilizotolewa usiku wa jana jijini London Uingereza.

Modric aliisaidia Real Madrid kutwaa klabu bingwa Ulaya pamoja na timu yake ya taifa ya Croatia kufika fainali ya kombe la dunia 2018 ambapo ilipoteza dhidi ya Ufaransa.

Orodha kamili ya washindi

MCHEZAJI BORA WA KIUME 

Nyota wa Real Madrid na Croatia, Luka Modric ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia wa FIFA 'FIFA Best Men's Player'. Amewashinda Cristiano Ronaldo na Mohamed Salah.

MCHEZAJI BORA WA KIKE
Nyota wa Brazil na klabu ya Orlando Pride, Marta Vieira da Silva ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa kike.

GOLI BORA
Mohamed Salah ameshinda tuzo ya goli bora la mwaka 'Fifa Puskas Award' kupitia goli lake alilofunga dhidi ya Everton.

KOCHA BORA SOKA LA WANAUME
Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps ameshinda tuzo ya kocha bora wa FIFA. Deschamps aliiwezesha Ufaransa kutwaa kombe la dunia 2018.

KIPA BORA 
Kipa wa Real Madrid na Ubelgiji ambaye msimu uliopita aling'aa na Chelsea Thibaut Courtois, ameshinda tuzo ya golikipa bora wa mwaka.

KOCHA BORA SOKA LA WANAWAKE
Kocha wa timu ya wanawake ya Olympique Lyon ya Ufaransa, Reynald Pedros, ameshinda tuzo ya kocha bora wa soka la wanawake.

MASHABIKI BORA
Mashabiki wa timu ya taifa ya Peru wameshinda tuzo ya mashabiki bora wa Fifa, 'The Fifa Fan Award'

TUZO YA FAIR PLAY 
Mchezaji Lennart Thy wa klabu ya VVV-Venlo ya Uholanzi ameshinda tuzo ya 'FIFA Fair Play'. Lennart alikosa mechi ya ligi kati ya timu yake dhidi ya PSV Eindhoven akiwa ameenda kujitolea msaada kwa mgonjwa wa kansa.

KIKOSI BORA CHA FIFA

1. David de Gea
2. Dani Alves
3. Marcelo
4. Raphael Varane
5. Sergio Ramos
6. N'Golo Kante
7. Lionel Messi
8. Luka Modric
9. Kylian Mbappe
10. Eden Hazard
11. Cristiano Ronaldo

No comments:

Post a Comment