Liverpool yawa mwiba mkali EPL, yaiadabisha Spurs kwenye dimba la Wembley - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 15 September 2018

Liverpool yawa mwiba mkali EPL, yaiadabisha Spurs kwenye dimba la Wembley

Klabu ya Liverpool imefanikiwa kuchomoza na ushindi wa jumla ya mabao 2 – 1 dhidi ya Tottenham mchezo wa ligi kuu ya England iliyopigwa hii leo siku ya Jumamosi.
Kwa sasa kikosi cha Liverpool kimeonekana kuwa mwiba mkali mbele ya timu pinzani baada ya kuonyesha makali yake kwa kucheza michezo mitano ya ligi bila kupoteza na hivyo kufikisha jumla ya pointi 15.
Waliyokuwa mashujaa katika mchezo huo ni Georginio Wijnaldum aliyeipatia Liverpool bao la kwanza dakika ya 39 na Roberto Firmino akiandika la pili dakika 54 wakati Spurs wakipata la kufutia machozi kupitia kwa Lamela dakika ya (90+3).
Katika kuelekea mchezo huo wadau wa soka wamekuwa wakimzungumzia nyota wa Spurs, Harry Kane kama mtu ambaye anaonekana kuchoka baada ya kucheza mechi nyingi ndani ya klabu na timu yake ya taifa.

No comments:

Post a Comment