Lemutuz Aikosoa Vibaya Miss Tanzania "Aibu ya Gari Mmejiletea Wenyewe Mlipoamua Kuwashambulia Miss Lake Zone" - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 9 September 2018

Lemutuz Aikosoa Vibaya Miss Tanzania "Aibu ya Gari Mmejiletea Wenyewe Mlipoamua Kuwashambulia Miss Lake Zone"William Malecela aka Lemutuz ameonekana kutofurahishwa na zawadi ya gari aliyopewa Miss Tanzania, Ameandika maneno makali kuhusu sakata hilo kupitia ukurasa wake wa instagram

Jisomee Hapa Chini:


From #lemutuz_superbrand - LIVE STRAIGHT TALK: THE ART OF SELF DESTRUCTIONS nimesema mara nyingi sana Adui wa binadam siku zote ni Binadam mwenyewe Miss Tanzania hii aibu ya gari mmejiletea wenyewe mlipoamua kuwashambulia Miss Lake Zone kwenye mitandao kwa sababu ya Gari lao la zawadi ambalo kwa kelele za mitandao mlitoa hukumu mbio mbio so wenyewe mkawa mmeweka standard ambayo binafsi nilitegemea mngeitimiza sasa na nyinyi mmerudia yale yale mliyoyakataa mlitegemea nini hasa?..nilichofanya ni kuwakumbusha tu matapishi yenu na mbwembwe mlizozipanda wenyewe mkasahau kwenye maisha TUNAVUNA TU TULICHOPANDA na leo mmevuna mlichopanda yaani Aibu ya Gari ambalo halifanani na hadhi yenu wenyewe mliyotuambia mnayo ...nimeona badala ya kujibu hoja baadhi yenu mnajaribu kunijibu matusi hahahahaha mimi huwa situkani I speak FACTS and let the Chips fall where they may ....binafsi mpaka sasa siamini kwamba mashindano ya Miss Tanzania yanaweza kufanyikia kwenye Jumba la Mikutano for sure hata Wa China waliotujengea hilo jengo la Mikutano leo wamejionea maajabu ya Dunia na watakuwa wametuma sana sms kwao kuwa Ukumbi wa Mikutano anaoutumia Rais na Viongozi wa Taifa kwa mikutano ya Kitaifa leo umetumika for Miss Tanzania ..hahahahaha please guys tuoneeni huruma wenzenu U know

Mashindano ya Miss Tanzania unayafanyiaje kwenye ukumbi ambao hauna nafasi ya kuongezwa kwa mbele maana ni lazima warembo waweze kutembea mbele nyuma kushoto na Kulia bila tatizo lakini leo mmewalazimisha kutembea kushoto na kulia na nyuma tu its is wrong tena Miss World wakisikia mnaweza kuingia matatizo makubwa sana ...na infact ingekuwa majuu washiriki wangeweza kuwashitaki na mashindano kurudiwa kwa kukosa kutembea kwa mbele kuonyesha vizuri urembo wao ...halafu now you know hakuna mtu anayeniamrisha kuandika au kufuta maana ninazo habari kuwa mmepiga simu kwa Viongozi wengi sana eti wanilazimishe nifute post zangu

...hahahaha...SIFUTI kama ambavyo hamkufuta ile barua yenu ya kuwadhalilisha waandaaaji wa Miss Lake Zone I hope mmeona jinsi inavyouma maumivu kama mliyowaletea wenzenu..MISS TANZANIA AIBU MLIYOVUNA LEO MLIPANDA WENYEWE kwenye Miss Lake Zone msilaumu mtu JILAUMUNI WENYEWE " Lemutuz


No comments:

Post a Comment