KUMBE HAUMWI!! RUNGU LA CAF LAMUWEKA BANKA WA YANGA NJE MPAKA SASA - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 4 September 2018

KUMBE HAUMWI!! RUNGU LA CAF LAMUWEKA BANKA WA YANGA NJE MPAKA SASA


Kiungo mpya wa klabu ya Yanga, Mohamed Issa Banka, amefungiwa kucheza soka na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa muda mwaka mmoja.

Banka amefungiwa kwa kosa la kufeli kwa vipimo ambavyo viliendeshwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) katika michuano ya CECAFA Challenge Cup, iliyofanyika mwaka jana nchini Kenya.

Taarifa zimesema kuwa timu ya Zanzibar na klabu ya Mtibwa walipewa majibu kuhusu vipimo hivyo ndiyo maana klabu ya Mtibwa Sugar haikuweza kumtumia kiungo huyo tangu Februari 2018.

Wakati huo Yanga ilifanikiwa kumsajili Banka bila kujua kama amefungiwa mwaka mmoja na CAF.

Wakati taarifa hizi hazijatoka, hivi karibuni uongozi wa Yanga ulisema kuwa Banka yupo kwao Zanzibar akiiguza majereha ya goti na ikitajwa kuwa sababu ya kuendelea kukosekana kwenye kikosi cha Yanga.

No comments:

Post a Comment