KOCHA SIMBA AINGILIA ANGA ZA AMUNIKE, ATOA NENO TFF - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 10 September 2018

KOCHA SIMBA AINGILIA ANGA ZA AMUNIKE, ATOA NENO TFF


Baada ya kukiwezesha kikosi cha Taifa Stars kwenda suluhu bila kufungana na Uganda The Cranes, Kocha Mkuu wa timu hiyo Emmanuel Amunike amemwagiwa sifa na Jamhuri Kihwelo 'Julio'.

Julio ambaye ni aliwahi kuifundisha na sasa ni Kocha Mkuu wa Dodoma FC, amesema Amunike ameanza kazi vizuri na ni vema akapewa muda zaidi kuliko kuanza kumkosoa mapema.

Kocha huyo anayependa sifa kuliko pesa, ameeleza kuwa Amunike ni bonge la Kocha hivyo kama akipewa muda ipasavyo anaweza akaifikisha timu mbali.

Aidha, Julio amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwa naye bega kwa bega ili kuhakikisha majukumu yake nayaenda vema kuiwezesha Stars kufika mbali.

"Huu ni mwanzo mzuri kwa Stars, Amunike anastahili pongezi na inabidi apewe nguvu na TFF ili kuiwezesha Stars kufika mbali" alisema.

No comments:

Post a Comment