KISA JEZI, RONALDINHO AITAKA BARCELONA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU KWA MESSI - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 5 September 2018

KISA JEZI, RONALDINHO AITAKA BARCELONA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU KWA MESSI


Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Barcelona na Brazil, Ronaldinho amesema mshambuliaji Lionel Messi akistaafu Barcelona wanatakiwa wasimpe mchezaji yeyote jezi yake.

Gaucho amesema kwa sasa hakuna mchezaji mwenye uwezo kama Messi pia ataweza kuipa heshima Barcelona kama yeye labda kwa badaaye sana na si hivi karibuni.

Kauli hiyo imekuja kutokana na mtazamo wa Gaucho kuamini Messi ndiye mtu wa mwisho kuipa heshima jezi hiyo akiwa na Barcelona hivyo hadhani kama atakuja mtu mwingine kuifanyia makubwa.

Gaucho ambaye aling'ara na Barcelona na akimuwezesha Messi kufunga bao lake la kwanza tangu aanze kukichezea kikosi cha kwanza, anaona Messi ndiye anastahili heshima ya mwisho kuvaa jezi hiyo na baada ya hapo istafishwe.

No comments:

Post a Comment