KIONGOZI WA JUU SIMBA AJIWEKA PEMBENI - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 11 September 2018

KIONGOZI WA JUU SIMBA AJIWEKA PEMBENI


Wakati zoezi la kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika klabu ya Simba likimalizika jana, Kaimu Rais wake, Salim Abdallah 'Try Again' ametangaza kujiweka pembeni.

Abdallah amesema sababu za kujiweka kando ni kuwaachia viongozi wengine waje na mawazo mampya ndani ya klabu ambayo inakuja na muundo mpya wa uongozi.

Kaimu huyo aliyekuwa anapewa nafasi kubwa zaidi ya kuchukua fomu, hakuweza kufika kwenye makao makuu ya klabu hiyo iliyo mitaa ya Msimbazi, Kariakoo kwa ajili ya kuchukua fomu hiyo.

Abdallah ameeleza kuwa wakati wa kuitumikia Simba umeshamalizika kama kiongozi lakini ataendelea kuwa mshauri kwa ajili ya kuiimarisha klabu kwa ujumla.

kiongozi huyo alichukua nafasi ya Evans Aveva ambaye alikuwa Rais wa klabu hiyo ambaye sasa ameshikiliwa na mahakama kutokana na makosa ya matumizi mabaya ya fedha.

No comments:

Post a Comment