Kimbunga Mangkhut Chaua Watu 30 Ufilipino - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 17 September 2018

Kimbunga Mangkhut Chaua Watu 30 Ufilipino

Takriban watu thelathini wameuawa baada ya kimbunga Mangkhut kupiga kaskazini mwa Ufilipino.

Wengi kati yao walikumbwa na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa.

Maeneo mengi ya kisiwa cha Luzon yamejaa maji, yakiwemo mashamba ambayo huzalisha mazao makuu nchini humo ya mpunga na mahindi.


Katika eneo hilo kunaelezwa kuwa kuna familia takriban elfu ishirini na sita na mia tatu na sitini na saba zilizoathirika ambazo zinahitaji msaada wa chakula na mahitaji mengine

Afisa wa kutoka shirika la msalaba mwekundu Chris Staines ameiambia BBC kuhusu kuwepo kwa hatari ya maporomoko ya udongo katika maeneo ya milima nchini Ufilipino ambayo yalikumbwa na kimbunga.

''Pepo za mansoon za kusini magharibi zimekwisha, na kusababisha eneo kuwa la maji kabla ya kimbunga cha Mangkhut kupiga, na kusabisha mvua zaidi''.

Jitihada za urejeshaji miundombinu zikiendelea
Akizungumza na BBC, mratibu wa shirika la misaada la Umoja wa mataifa nchini Ufilipino, Ola Almgren ameeleza changamoto zinazotakiwa kushughulikiwa na mashirika ya misaada.

''Kimbunga hiki kimesabisha madhara makubwa mawili :upepo wake na maji. Tunasubiri kusiki zaidi katika maeneo mengine ni kwa namna gani yameathirika na mvua ambayo ilibebwa na kimbunga.Hivyo tunachokifanya sasa ni kufanya tathimini kuhusu misaada, na uharibifu.Tunachukua hatua kadiri mazingira yanavyotuhitaji kwa kutumia rasilimali tulizonazo.Tunajiandaa kuongeza jitihada kukabili hali hii tukiwa na rasilimali za kimataifa ambazo zitahitajika''.

No comments:

Post a Comment