KIBA AWASHUSHA PRESHA MASHABIKI COASTAL UNION - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 16 September 2018

KIBA AWASHUSHA PRESHA MASHABIKI COASTAL UNION


Mshambuliaji wa Coastal Union ya Tanga, Ali Kiba amewashusha presha mashabiki wake ambao hawajamuona akianza mikikimikiki ndani ya timu hiyo kwenye michezo minne kwa kusema kuwa hana haraka ya kucheza kwa sasa na badala yake anausoma mchezo jinsi ambavyo unaenda.

Kiba ambaye ameweka rekodi katika usajili wa msimu huu ya kuwa msanii wa muziki ambaye amejiingiza kwenye soka amekosa mechi za Coastal Union dhidi ya Lipuli FC, Biashara United, KMC na African Lyon.

Kwa mara ya kwanza Kiba ambaye pia ni mdhamini wa timu hiyo, ameliambia Spoti Xtra kuwa; “Ifahamike kuwa haina haraka ya mimi kucheza kwani mpira una njia na kanuni zake ambazo mtu unatakiwa uzijue.”

“Ni lazima uzijue vizuri hizo na siyo unakurupuka na kuingia uwanjani, niko vizuri kabisa ila kwa sasa natafuta kuielewa timu kabla ya kuonekana uwanjani kwenye mechi zijazo za timu yangu,” alisema Alikiba ambaye ni shabiki wa kulia machozi wa Yanga.

No comments:

Post a Comment