KAGERE AMFUNIKA BEKI MAN UNITED - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 15 September 2018

KAGERE AMFUNIKA BEKI MAN UNITED


Mshambuliaji wa Simba, Mnyarwanda, Meddie Kagere, amemfungukia beki wa timu ya taifa ya Ivory Coast na Klabu ya Manchester United ya England, Eric Bailly baada ya wawili hao kupambana Jumapili iliyopita.

Kagere na Bailly walipambana kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Mataifa Afrika (Afcon), michuano itakayofanyika mwakani nchini Cameroon ambapo wenyeji Rwanda walipoteza kwa mabao 2-1.

Baada ya mchezo huo wa Kundi H ambao bao pekee la Rwanda lilifungwa na Kagere huku yale ya Ivory Coast yakifungwa na Jonathan Kodjia na Max-Alain Gradel, picha za wawili hao zikaanza kusambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii zikiwaonyesha wakipambana ambapo moja ya picha hiyo inamuonyesha Bailly akiwa amepata jeraha la paja kutokana na kumkaba Kagere.

“Bailly ni beki mzuri sana, ametulia na anaifanya kazi yake kisawasawa. Niliweza kupambana naye, lakini nashukuru nikapata nafasi ya kufunga nikafanya hivyo ingawa bao hilo halikuweza kutusaidia kupata ushindi kutokana na kupoteza kwa mabao 2-1,” alisema Kagere. 

Kuhusu mtazamo wake kwa Ligi Kuu Bara. “Kikubwa ambacho kinasaidia kupata matokeo kinajulikana hasa kwa timu kushirikiana na kuelewana ndani na nje.

“Tunaendelea kupambana na kila nikipata nafasi ya kucheza nitahakikisha nasaidia timu kuondoka na pointi bila kujali nani atakayefunga kwani nafanya kazi kwa ajili ya timu hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti,” alisema Kagere.

No comments:

Post a Comment