Jezi mpya za Wizkid zinazotengenezwa na kampuni ya Nike zaisha sokoni ndani ya dakika 10 (+picha) - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 10 September 2018

Jezi mpya za Wizkid zinazotengenezwa na kampuni ya Nike zaisha sokoni ndani ya dakika 10 (+picha)

Msanii wa muziki kutoka Nigeria, Wizkid amejikuta akitimiza malengo yake ya kibiashara kwa muda mfupi  baada ya jezi zake mpya zenye logo ya StarBoy kuingia sokoni kwa siku ya kwanza na kununuliwa zote ndani ya dakika 10.

Wizkid
Wizkid amethibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika “That was fast! Sold out in 10mins!🌏🌏🌏🌹🦅 Love u all like crazy!😭😭😭 God working harder than satan!❤️❤️❤️😇“.
Jezi moja ya StarBoy inauzwa Euro 64.95 ambayo ni sawa na laki 1.7 . Jezi hizo zimepokelewa vizuri sana na mashabiki wa Wizkid na huenda lengo lake la kujenge shule likakamilika haraka.
Nike imeingia mkataba wa makubaliano ya kibiashara na Wizkid kutengeneza Jezi ambazo zitakuwa na logo ya StarBoy, na leo Nike ndio wameingiza jezi hizo rasmi sokoni.

No comments:

Post a Comment