Hans Pluijm awazuga Simba na Yanga - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 3 September 2018

Hans Pluijm awazuga Simba na Yanga


Kocha wa klabu ya soka ya Azam FC, Hans Pluijm ameweka wazi kuwa ubingwa wa msimu huu sio kipaumbele cha waajiri wake - Lakini kwa kauli hiyo ni kama anawazuga Simba na Yanga.

Azam imeanza vizuri michezo yake ya mwanzo ya ligi kuu msimu huu kwa kushinda michezo yote miwili waliyocheza dhidi ya Mtibwa FC na Ndanda FC kwenye uwanja wao wa Azam Complex.

“Sijui kama Azam wamenileta kuja kutwaa taji msimu huu, ila kama mwalimu wa timu unahitaji kuonyesha uwezo na mawazo yako kwa wachezaji ili waonyeshe ubora wao binafsi na ubora wa timu,” amesema kocha Pluijm.

“Nafikiri wanahitaji zaidi kuona wachezaji wakicheza kwa kujituma kwa bidii na kuonyesha kuwa wanahitaji kushinda hilo ndiyo jambo bora na kama kutwaa ubingwa kutakuja kuonekana mwishoni mwa msimu,” ameongeza.

No comments:

Post a Comment