Hali ya Ommy Dimpoz Yaimarika Atoka Afrika ya Kusini na Kutua Kenya - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 10 September 2018

Hali ya Ommy Dimpoz Yaimarika Atoka Afrika ya Kusini na Kutua Kenya

Hii inaweza kuwa habari njema kuliko zote kwa mashabiki wa msanii Ommy Dimpoz ambae alikuwa mgonjwa sana hapo siku za nyuma na kuonekana kudhoofika sana kutokana na ugonjwa wa koo alikuwa ameupata huku sababu kubwa ikisemwa kuwa ni kutokana na sumu aliyowahi kunywa katika kinywaji.

Msanii Ommy Dimpoz sasa ameshatoka kule alipokuwa ambapo inawezekana kulikuwa kukiwapa watu wengi wasiwasi kutokana na ukaribu wa sehemu hiyo, Ommy Dimpoz ssasa yuko nchini Kenya na ameshatoka Afrika ya Kusini ambapo ndipo alipokuwa akipatiwa matibabu hayo.

Hata hivyo kwa picha mpya ilisambaa sana katika mitandao, msanii huyo amebadilisha muonekana huku muonekano wake ukionekana kuimarika na wa kupendeza zaidi na umekuwa ukitia moyo kulingana na hali aliyokuwa nayo hapo awali.


Pamoja na kwamba haijajulikana  dhumuni la safari yake ya Kenya lakini mashabiki wamefarijika na kusema labda sasa ni wakati wa msanii huyo kurejea nyumbani na kuungana nae.

No comments:

Post a Comment