GUARDIOLA, RABIOT, ASENSIO, MAGUIRE, RAKITIC: TETESI KUBWA ZA SOKA ULAYA LEO ALHAMIS - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 6 September 2018

GUARDIOLA, RABIOT, ASENSIO, MAGUIRE, RAKITIC: TETESI KUBWA ZA SOKA ULAYA LEO ALHAMIS


Kiungo wa kati wa Manchester United mwenye miaka 25 Paul Pogba hawezi kulazimisha kukama kwake mwezi Januari. (Mirror)

Liverpool wamefanya mawasiliano na mama na pia ajenti kwa kiungo wa kati wa Paris St-Germain mwenye miaka 23 Adrien Rabiot. (ESPN)

Meneja wa Manchester City' Mhispania Pep Guardiola amepiga marufuku simu kwenye maeneo ya kufanyia mazoezi ya klabu hiyo. (Daily Mail)

Mlinzi wa Tottenham mweneye miaka 31 Jan Vertonghen anatarajia klabu kuongeza mkataba wake kwa mwaka mwingie mmoja. (Evening Standard)

Mlinzi wa England na Leicester Harry Maguire, 25, anasema haelewi jinsi mataifa ya uefa hufanya kazi. (Telegraph)


Aliyekuwa kiungo wa kati wa Norwich na Jamhuri ya Ireland Wes Hoolahan, 36, anafanya mazoezi na West Brom na atijiunga kama mchezaji huru. (Eastern Daily Press)

Kiungo wa kati wa Barcelona raia wa Croatia mwenye miaka 30 Ivan Rakitic anasema vilabu vikubwa vilikuwa vinataka kumsaini msimu huu, lakinia aliamua kubaki Uhispania. (Novi List - in Croatian)

PSV wanataka kumsaini kiungo wa kati wa Real Monarchs mmarekani Richard Ledezma 17, (Eindhovens Dagblad - in Dutch)


Klabu ya Ureno ya Benfica itapigwa marufuku ya kucheza kwa hadi miaka mitatu baada ya kulaumiwa kwa uhalifu unaohusu kuingilia mifumo ya sheria wa nchi. (Correio da Manha - in Portuguese)

Real Madrid wamempa ofa mshambuliaji Marco Asensio jesi namba 7 ya klabu hicho lakini mchezaji huyo wa miaka 22 amekataa. (Cope - in Spanish)


Fulham wanataka kumpa kipa raia wa England mwenya miaka 26 Marcus Buttinelli mkataba mpya. (Sun)

Kutoka BBC

No comments:

Post a Comment