FIFA watangaza majina matatu ya wachezaji watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa dunia, Lionel Messi atoswa - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 3 September 2018

FIFA watangaza majina matatu ya wachezaji watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa dunia, Lionel Messi atoswa

Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) limetangaza majina matatu ya wachezaji watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2017/18, ambapo kwenye majina hayo mshambuliaji wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi ametoswa kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2006.
Majina ya wachezaji hao ni Luka Modric (Real Madrid), MO Salah (Liverpool) na Cristiano Ronaldo (Juventus). Majina hayo ndiyo yale yale yaliyotangazwa kwenye tuzo ya mchezaji bora wa kiume barani Ulaya.
Maswali mengi yameibuka mitandaoni kwanini Lionel Messi ameachwa kwenye orodha hiyo, ile hali yeye ndiye mfungaji bora barani Ulaya msimu uliopita na ameisaidia timu yake ya Barcelona kuchukua ndoo ya La Liga na kombe la Mfalme ‘Copa Del Rey’.
Bado haijajulikana wameangalia nini kwani mchezaji kama MO Salah timu yake ya Liverpool haijachukua kombe lolote huku yeye akiibuka mfungaji bora wa EPL.

No comments:

Post a Comment