FEI TOTO AMPONZA AJIBU YANGA - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 5 September 2018

FEI TOTO AMPONZA AJIBU YANGA


Kocha Mkuu wa Yanga, Mkongomani, Mwinyi Zahera amefurahishwa na umakini wa upigaji pasi safi zilizonyooka wa kiungo wake, Feisal Salim ‘Fei Toto’ huku akimtaka kiungo mshambuliaji, Ibrahim Ajibu kumuiga nyota huyo.

Kauli hiyo aliitoa baada ya kumalizika kwa mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda ambayo ilimalizika kwa Yanga kufungwa bao 1-0, huku Ajibu akicheza namba 10 ambayo Zahera amekuwa akimpanga Fei Toto.

Ajibu ambaye hivi karibuni alikuwa hana nafasi ya kudu­mu katika kikosi cha kwanza cha Zahera alionyesha kiwango kizuri sana kwenye mechi hiyo.

Akizungumza na Championi Juma­tano, Zahera al­isema mshambuliaji huyo ana tatizo kubwa la kupoteza pasi nyingi katika mechi ambalo hataki kuona likiendelea kwenye michezo ijayo ya ligi.

“Siku zote upote­zaji wa pasi una­tokana na mchezaji kutokuwa makini, ili mchezaji apige pasi safi ni lazima awe makini.

No comments:

Post a Comment