FC Barcelona watoa kipigo cha ‘Mbwa koko’ La Liga, Tottenham Spurs ikiangukia pua EPL - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 2 September 2018

FC Barcelona watoa kipigo cha ‘Mbwa koko’ La Liga, Tottenham Spurs ikiangukia pua EPL

Klabu ya Barcelona imeendeleza ubabe kunako ligi kuu soka nchini Hispania (La Liga) kwa kuichabanga klabu ya SD Huesca ambayo imepanda daraja msimu huu kwa goli 8-2 .

Lionel Messi na Luis Suarez wakishangilia
SD Huesca ndio walikuwa wa kwanza kucheka na nyavu za Barcelona kabla ya Lionel Messi kusawazisha goli hilo, na mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Barca walikuwa wanaongoza goli 3-2 .
Magoli ya Barcelona yamefungwa na L. Messi x2, L. Suarez x2, O. Dembele, Rakitic,  Alba huku goli la moja likiwa la kujifunga kutoka kwa beki wa Huesca, Jorge Pulido.
Kwa matokeo hayo Barcelona wanakaa kileleni kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Hispania.
Kwa upande mwingine, klabu ya Tottenham Spurs ya Uingereza imepokea kichapo cha kwanza kunako ligi kuu nchini humo (EPL) kwa kukubali kunyukwa goli 2-1 dhidi ya Watford FC.

No comments:

Post a Comment