EVERTON KUBADILI JEZI KWA AJILI YA AFRIKA, WATAKUWA WAKIIVAA WEST HAM UNITED KESHI - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 15 September 2018

EVERTON KUBADILI JEZI KWA AJILI YA AFRIKA, WATAKUWA WAKIIVAA WEST HAM UNITED KESHIWachezaji wa timu ya Everton FC watakuwa wamevalia jezi zenye nembo tofauti kesho  Jumapili hii wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani dhidi ya timu ya West Ham United kwenye michezo ya Ligi kuu inayoendelea.

Washirika wakuu wa timu ya Everton, kampuni ya ubashiri wa michezo SportPesa, watatoa jina lao na nembo ya kifuani kwenye jezi za timu bhiyo na kuweka “Kits For Africa.


Mechi hiyo ambayo itaonyesha moja kwa moja na kushuhudiwa na mamilioni ya mashabiki ulimwenguni kote, itakuwa na mabadiliko ya nembo ambayo itasaidia kuhamashisha mradi wa kutoa jezi na kuunga mkono timu ndogo ndogo za mpira wa miguu barani Afrika.


SportPesa na Everton zimekuwa zikikusanya jezi ambazo zinatolewa na mashabiki, wachezaji pamoja na wadau wengine wakati wa mechi za Nyumbani kwa mwezi wa Agosti na Septemba na watazingawa barani Afrika kwa timu ambazo hazina uwezo pamoja na kwa watu binafsi ambao wanapenda mchezo wa mpira wa miguu.


Mechi hiyo ya jumapili dhidi ya West Ham United ambayo ipo chini kocha Manuel Pellegrini’s ndio fursa ya mwisho kwa mashabiki kutoa jezi zao na mashabiki wanaombwa kuleta jezi za zamani au vile ambazo hazijatumikwa na kuziweka kwenye eneo la Fan Zone ambalo limeandikwa ‘Kits For Afrika’ ambazo kuziweka kwenye moja ya stoo za Everton.

Kwenye makusanyiko hayo ambayo yatakuwa yanalindwa na wafanyakazi wa SportPesa, ambao watazikusanya tayari kwa kusambaza kwa wenye mahitaji barani Afrika. Bidhaa yeyote inayoendana na vifaa vya michezo itakubalika ikiwemo jezi, vitabu, soksi, suruali za michezo – ukarimu wa mashabiki wa Everton msimu uliopita ulisababisha kupatikana kwa tani tatu za jezi ambazo zilisabazwa barani Afrika.


Mashabiki watakuwa na uwezo wa kuendelea kutoa jezi zao kupitia jukwaa la Everton 1 au Everton 2 na pia wanaweza kutuma kupitia sanduku la posta CSM Live – Kits For Afrika, Unit D1, Grafton Way, West Ham Industrial Estate, Basingstoke, RG22 6HY.

‘Kits For Afrika’ (K4A) ni kampeini inayoendelea ya SportPesa yenye nia ya kukuza mpira wa miguu barani Afrika kuanzia ngazi ya chini kwenye nchi ambazo SportPesa inafanya kazi tangu kuanzisha kwa kampuni 2014 ambayo imeweza kukua kwa haraka na kujijengea heshima kwa Jamii kama moja ya bidhaa bora barani Afrika na duniani pia.
Ikiwa ndio kampuni inayoongoza barani Afrika kwa ubashiri wa michezo, SportPesa imekuwa ikibadilisha maisha ya wateja wake pamoja na kusaidia miradi mbali mbali kwenye Jamii.

No comments:

Post a Comment