BREAKING: SIMBA WATAJA TAREHE YA UCHAGUZI MKUU, YATAKAYOZINGATIWA NI HAYA - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 2 September 2018

BREAKING: SIMBA WATAJA TAREHE YA UCHAGUZI MKUU, YATAKAYOZINGATIWA NI HAYA


Na George Mganga

Uongozi wa Simba kupitia Kamati ya Uchaguzi, umeitangaza Novemba 3 2018 kuwa ndiyo siku maalum ya uchaguzi mkuu wa klabu hiyo.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Boniface Lihamwike, amesema nafasi pekee zinazowaniwa ni ya Rais pamoja na wajumbe watano watakaoingia kwenye bodi ya klabu.

Lihamwike ameeleza kuwa Mwanachama atakayewania nafasi ya Urais ndani ya klabu anapaswa kuwa na kiwango cha elimu ya Shadaha kutoka Chuo Kikuu 'Degree' na hii ni kutokana na kutokana na mabadiliko ya katiba mpya iliyopitishwa mwaka 2018.

Mbali na shahada kwa Mwenyekiti, katika orodha ya wajumbe hao watano, mjumbe mmoja atapaswa kuwa na shahada ya kwanza ya Chuo Kikuu huku wengine wakiwa na kiwango cha elimu ya kidato cha nne.

Katika wajumbe hao wanne, Lihamwike amesema mmoja wao anapaswa kuwa mwanamke ili kuleta usawa wa kijinsia katika uwajibikaji wa kazi za klabu.

No comments:

Post a Comment