BOCCO NDIYO BASI TENA TAIFA STARS - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 4 September 2018

BOCCO NDIYO BASI TENA TAIFA STARS


Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Kelvin Sabato ‘Kiduku’, amesema anauona mwisho wa straika wa Simba, John Bocco katika kikosi cha Taifa Stars, baada ya yeye kuitwa kikosini hapo.

Siku chache zilizopita, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mnigeria, Emmanuel Amunike, alimwita Kiduku pamoja na wachezaji wengine watano katika

Kikosi hicho kuchukua nafasi za wachezaji sita wa Simba akiwemo Bocco, ambao aliwatimua kwenye kambi ya kujiandaa na mchezo wa kufuzu Afcon dhidi ya Uganda utakaochezwa Septemba 8.

Kwa mujibu wa Championi, Kiduku alisema kuwa baada kupata nafasi hiyo, amejipanga kuhakikisha anamshawishi

Amunike ili aendelee kumuita katika kikosi hicho na kuachana na Bocco.

“Kufa kufaana, hivyo ndivyo unavyoweza kusema kwani nimefurahi sana kuitwa katika kikosi cha Taifa Stars kuchukua nafasi ya Bocco ambayo naamini nitaitendea haki ili niendelee kuitwa katika kikosi hicho.

“Uwezo wa kufanya hivyo ninao kutokana na jinsi ambavyo nimekuwa nikicheza kwa kujituma uwanjani lakini kupambana kuhakikisha naongoza timu yangu kupata ushindi, kwa hiyo Bocco inabidi ajipange upya,” alisema Kiduku ambaye kwa sasa ndiye mshambuliaji wa kutumainiwa katika kikosi cha Mtibwa Sugar.

Alipotafutwa Bocco ili kuzungumzia majigambo hayo ya Kiduku hakupatikana kutokana na simu yake ya mkononi kuita tu bila kupokelewa.

No comments:

Post a Comment