Balozi Seif asema SMZ itaendelea kuboresha Sekta ya Elimu kwa hili - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 6 September 2018

Balozi Seif asema SMZ itaendelea kuboresha Sekta ya Elimu kwa hili


Na.Thabit Madai, Zanzibar.

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea na jitihada za kuimarisha miundombinu na kuweka mazingira bora yatakayo wezesha kuinua viwango vya ufaulu kwa wanafunzi wa skuli za msingi na sekondari.

Hayo yameelezwa na Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akiwahotubia wananchi katika hafla maalum ya kuwakabidhi zawadi za laptop wanafunzi 96 waliopata ufaulu wa division 1 kwa mwaka 2018 katika mkoa wamjini magharib Unguja.

Balozi Seif Alisema jitihada za serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ya kusimamia vyema na kutekeleza mipango na mikakati ya kisekta kwa lengo kuleta maeendeleo endelevu katika sekta ya elimu Zanzibar.

“sekta ya elimu ni miongoni mwa sekta zilizopewa kipaumbele sana na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar  hivyo tutaendelea kusimamia vyema sera na kanuni  mbali mbali ili  kuinua sekta hii kwa kuongeza ufaulu kwa wanafunzi skuli za msingi na sekondari“ alisema Balozi Seif.

Aidha alisema  jitihada hizo za Serikali zinakwenda sambamba na utekelezwaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya mwaka 2015-2020.


Balozi Seif alitoa pongezi kwa Wizara ya elimu na mafunzo ya amali Zanzibar pamoja uongozi wa mkoa wa mjini magharib kwa  jitihada mbali mbali za kuinua elimu na kufanikiwa kuongeza ufaulu wa wanafunzi katika mtihadi wa kidatio cha sita.

“Ni jambo la kutia moyo na faraja kubwa kuona kuwa mkoa wa mjini magharib na zanzibar kwa ujumla kuwa imeondoka katika idadi ya skuli ya mikoa yenye skuli nyingi zilizofanya vibaya Tanzania hivyo nitoe pongezi kwao na uongozi wa wizara kwa kuweza nguvu nyingi katika suala hili” alisema Balozi Seif Ali Iddi.

Kwa upande wake waziri wa elimu na mafunzo ya Amali Zanzibar Rizik Pembe Juma akaishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Uongozi mahiri wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein kwa kutoa fursa 30 za Mafunzo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wa Zanzibar wanaomaliza vyema masomo yao ya Darasa la 14.

Alisema  Serikali inaendelea kujali jitihada za Wanafunzi hao na kuahidi kuongeza fursa nyengine kadri hali ya Uchumi itaklavyoruhusu.

Nae Mkuu wa mkoa wa mjini magharib Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud alisema hatua hiyo ya utoaji zawadi kwa vijana hao imekuja kutokana na ahadi aliyoitoa wakati alipokutana na wanafunzi wa skuli 17 za mkoa wa mjini magharib  waliokuwa wakijiandaa na mitihani mnamo mwezi April mwaka huu ambapo aliahidi kutoa kompyuta aina ya  laptops watakaopata ufaulu wa daraja la kwanza (Division one) katika mitihani yao.

Alisema ahadi hiyo ililenga kuwahamasisha wanafunzi hao kufanya bidii katika masomo yao na kufanikiwa kupata matokeo mazuri ambayo hajawahi kupatikana katika kipindi kirefu ndani na nje ya mkoa huo.

aidha aliwataka wanafunzi hao kuweza kuzitumia komputa hizo kwa kujiendeleza kimasomo na si kwa matumizi mengine ambayo hayajakusudiwa.

Hafla hiyo fupi ya kuwazawadia  Laptop Wanafunzi 96 wa Skuli 17 za Kidato cha sita Mkoa Mjini Magharibi imehudhuriwa pia na wadau mbali wa Sekta ya elimu wakiwemo pia Wawakilishi wa Jumuiya za Kiraia, Taasisi za Kujitolea pamoja na Viongozi wa Kisiasa kutoka  Vyama mbali mbali Nchini.

No comments:

Post a Comment