BAADA YA POGBA KUMCHANA LIVE MOURINHO, VITA YAANZA UPYA TENA - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 25 September 2018

BAADA YA POGBA KUMCHANA LIVE MOURINHO, VITA YAANZA UPYA TENA


Mahusiano ya Kocha wa Manchester United Jose Mourinho na kiungo wa klabu hiyo Mfaransa, Paul Pogba yanaendelea kuwa mabaya.

Hatua hiyo imekuja baada ya Pogba kukosoa mbinu za kujilinda za kocha Mourinho waziwazi.

Baada ya mchezo dhidi ya Wolves ambao walitoa sare ya 1-1, Pogba alisema walitakiwa kushambulia zaidi wakiwa katika Uwanja wa nyumbani ila kwa kuwa yeye si kocha hana uwezo wa kuwaambia wachezaji wenzake washambulie.

Wawili hao wamekuwa kwenye vichwa vya vyombo mbalimbali vya habari kwa muda mrefu jambo ambalo linatilia shaka uwezekano wa kuendelea kucheza United katika siku za usoni.

No comments:

Post a Comment